Nordic Journal of African Studies (Dec 2013)

Muundo wa Kimofo-Sintaksia wa Kitenzi (Kt) cha Kinandi kwa Mtazamo wa Kiunzi cha Kanuni Finyu (Kkf)

  • Hellen Chesang Barno

DOI
https://doi.org/10.53228/njas.v22i4.155
Journal volume & issue
Vol. 22, no. 4

Abstract

Read online

This study investigated morphosyntactic levels of verb phrase structure (VP) of Nandi language using Minimalist Program (MP). The components of MP that were used included: feature checking, merge, move and also X-bar theory. Nandi sentences were generated and verified by native speakers of the Nandi language. The findings of this study show that the agreement subject (AgrS) can be projected in the functional nodes of the agreement subject 1 (AgrS1) while the agreement object (AgrO) can be projected in the functional nodes of the agreement object 1 (AgrO1). AgrS comes before the root of the verb in present tenses and after the root in the past and future tenses. The negative elements in a verb change depending on number and person. In conclusion, Nandi verb has morphosyntactic features which can be projected in the functional nodes in the VP structure. Ikisiri Utafiti huu ulichunguza muundo wa mofosintaksia wa Kikundi Kitenzi (KT) cha Kinandi katika viwango vya mofo-sintaksia na uliongozwa na Kiunzi cha Kanuni Finyu (KKF). Vipengele vya nadharia hii vilivyotumika ni uhakikishaji, uunganishaji, usogezaji na pia nadharia ya Eksibaa. Sentensi za Kinandi zilizalishwa na kuhakikishwa na wathibitishaji wazawa na wasemaji wa lugha ya Kinandi. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kuwa kipatanishi kiima ni cha lazima na huchomozwa katika kielelezo tungo katika sehemu ya kiuamilifu ya Kipatanishi Kiima (KptK)1. KptK hutokea katika sehemu mbili kulingana na wakati husika; mwanzoni katika wakati uliopo (Wkpo) na baada ya mzizi (mzz) wa kitenzi katika wakati uliopita na wakati ujao (Wkjo). Kwa upande mwingine, kipatanishi yambwa (KptY) hutokea mwishoni mwa kitenzi. Aidha, kibainishi cha ukanushi (Kns) hubadilika kutegemea idadi na nafsi (Nfs). Kwa kuhitimisha, imebainika kwamba KT cha Kinandi kimeundwa na vipashio vya kimofosintaksia na kwamba vinaweza kuchomozwa kwenye vifundo amilifu.